Breaking News

TAKUKURU Mkoa Wa Temeke Yamdaka Mhandisi Majenzi Kwa Rushwa Ya Ngono.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa temeke bi. Pilly Mwakasege akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Dec 5 jijini dar es salaam. 

Dar es salaam:
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  mkoa wa temeke (TAKUKURU) inamshikilia Mhandisi Leornard Mkaka wa kampuni ya MASK and SONS kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa na. 11/2017.

Akizungumza mapema leo jijini dar es salaam mkuu wa takukuru mkoa wa temeke bi. Pilly Mwakasege alisema mara baada ya kupokea taarifa na kujiridhisha kuwepo kwa mazingira ya rushwa ivyo kuandaa mtego wa rushwa ya ngono na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.

"Mara baada ya kupokea taarifa na kujiridhisha kuwepo kwa viashiria vya rushwa ya ngono maofisa wake waliandaa mtego wa rushwa ya ngono na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Nara Beach logde iliyopo kibada wilaya ya kigamboni".

Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa 
raia mwema mtuhumiwa ambaye ni mhandisi wa kampuni ya Mask and Sons ambayo ilipewa kazi ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Halmashauri ya Temeke katika kata ya Tuangoma mtaa wa Masaki aliomba rushwa ya ngono ili amwekee mlalamikaji Calvat mbele ya nyumba anayoishi kufatia kuaribika barabara ya kwenda kwake kutokana na ujenzi unaoendelea katika eneo hilo. 

Aidha bi Mwakasege ametoa wito kwa wa wananchi kuwa wajasiri na kujitokeza kuripoti vitendo vya rushwa kwa kupiga namba ua bure 113 au kufika ofisi ya takukuru pamoja na kutojihusisha na vitendo hivyo. 

Mara taratibu za kisheia zitakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka chini ya kifungu cha 25 cha sheria ya kupambana na rushwa Na. 11 ya mwaka 2017.