Breaking News

11 WAPITISHWA KUWANIA UONGOZI NGOME YA VIJANA ACT-WAZALENDO DAR

SEKRETARIETI ya Ngome ya Vijana Taifa ya Chama Cha ACT-Wazalendo imepitisha wagombea 11 kati ya wagombea 12 waliochukua na kurejesha fomu kwa nafasi saba za uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mchakato huu wa uchaguzi unafanyika baada ya Oktoba 10 mwaka jana Chama Cha ACT-Wazalendo kuvunja uongozi wa Mkos wa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa Ngome ya Vijana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Ngome ya Vijana,Wakili Victor Kweka amewataja wagombea waliopitishwa ngazi ya Mwenyekiti wa Mkoa ni Felex Ferdinand Kamugisha na Rahim Yazid Twaibu.

Nafasi ya Katibu wa Mkoa Ngome ya Vijana ni Mwantum Ramadhani Gogo, Salumu Saidi Mkwanda na Shabani Selemani Kabena, Katibu Mipango na Uchaguzi ni Ally Justine Ng’wihend na Hamidy Mmanga Omary.

Wengine ni Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma Mohammed Hassan Saidi, Mweka Hazina ni Hawa Omary Marock, Mjumbe mmoja mwanamke wa Kamati ya Uongozi Salma Khatibu Rashid na Mjumbe mmoja mwanaume wa Kamati ya Uongozi Kassim Salum Mtigile.

Wakili Kweka alisema mgombea mmoja Jamaica Adam Kyando ameenguliwa kugombea kwa sababu za kiumri kwa mujibu wa mwongozo wa Ngome ya Vijana na Kanuni za Uchaguzi wa Ngome ya Vijana kijana ni kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35.

Amesema kutokana na Kyando kuwa na umri wa miaka 40 amekosa sifa za kuwa mgombea kwa nafasi aliyoomba ambayo ni Mweka Hazina wa Ngome ya Vijana wa Mkoa wa Der es Salaam.

Aidha wakili kweka aliongeza kuwa kesho Machi 12, 2022 kutakuwa na mdahalo kubwa Makao Makuu ya Chama hicho utakao wakitanisha wagombea wa nafasi ya uenyekiti  kuanzia saa 10:00 jioni.