WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA DUBAI KUNUNUA NA KUUZA BIDHAA ZAO KUPITIA MTANDAO WA DU BUY
Timoth Marko
Katika kuhakisha sekta ya Biashara kwa njia ya Mtandao inakuwa na tija na kujenga uchumi wa kijitali, Kampuni ya Du Buy ya kutoka nchini Dubai imehaidi kukuza ushirikiano kati ya makampuni ya Kitanzania katika kuuza na kununua bidhaaa za kitanzania na zakutoka nchi hiyo.
Akizungumza nawaaandishi kwenye makubaliano ya wizara ya viwandana biashara na kampuni Du Buy jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa wizara ya Uwekezaji Viwanda na biashara Profesa Godius kahyara amesema Mtandao wa DuBuy.com utawawezesha wafanyabishara wa nchi hizi mbili kuweza kununua na kuuza bidhaa kupitia mtandao huo.
'"Leo tumeingia makubaliano ya mikataba 38 yenye thamamani ya dolaza kimarekani bilioni 80 sawa fedhaza kitanzania trion16" Alisema Profesa Kahyra
Prof. Kahyara alisema sekta binafsi na sekta ya umma ndio kipaumbele katika dira ya maendeleo ya taifa 2025.
Alisema mfumo wa kidijitali utasaia kuwezesha kuleta mabadiliko makubwa katika uchumi na makusanyo ya maduhuli ya serikali.
"Mikataba hii 38 yenye thamani Trilioni 16 ni mwendelezo wa makubaliano ya mkutano wa dubai Expo lengo lake ni kukuza biashara baina ya dubai na Tanzania". Aliongeza Profesa Kahyra.
Aisha Profesa kahyra aliongeza kuwa Tanzania imejaliwa kuwa na rasimali bahari ambapo faida zake ni kubwa katika makusanyo ya kodi.








