ACT WAZALENDO YALITAKA JESHI LA POLISI KUMWACHIA WAKILI PETER MADELEKA NA KUJIBU HOJA ZAKE
Chama cha ACT Wazalendo kimelitaka jeshi la polisi kumwachia mara moja wakili Peter Madeleka na kulitaka jeshi hilo kuchukua hatua ya kuchunguza hoja alizozitoa juu ya kitishiwa maisha.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo 21 april na waziri kivuli wa mambo ya ndani ya nchi, Ndg. Mbarala Maharagande imesema kuwa jeshi la polisi linapaswa kujibu hoja ambazo zilizotolewa na wakili huyo na kuachana na vitisho na ukamataji.





