Breaking News

SERIKALI YAENDELEA KUCHUKUA MAONI YA WADAU WA USAFIRISHAJI KUHUSU MAPENDEKEZO YA KUPANDA KWA NAULI

Serikali  imesema itaendelea kuangalia mapendekezo  ya upandaji wa nauli baada ya hatua zote za uchakataji wa mapendekezo hayo yaliyotolewa na wadau wa sekta ya usafirishaji  kufikiwa.

Akizungumza  katika kikao cha  wadau wa wa usafirishaji uliowajumuisha madereva wa magari ya mikoani na wamiliki wa magari hayo,Katibu wa Wizaraya uchukuzi Gabriel Migire amesema kuwa sekta hiyo ya usafirishaji kwa njia ya barabara  imekuwa ikichangia kwenye uchumi kwa kiwango kikubwa.

“Kumekuwepo malalamiko hasa kwawadau wa usafirishaji  ndipo Mheshmiwa Rais Samia Suluhu Hassan amenitaka nikutanenanyi ilikuwezakujadili mkanganyiko wa kisheria hivyo kama wadau lazima tukaechini tuwezekutafuta ufumbumbuzi “.Alisema  Katibu Mkuu Migire.

Migire alisema kikao cha wadau wa sektaya usafirishaji  wa mabasi ya Abiria ya mikoani kimetokana na Maagizo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu Hassan hivikaribunikutokana mkanganyiko wa sheria 19 ya mwaka 2019 katika sekta hiyo.

Aliongeza kuwa kikao hicho kinalenga kupunguza na kuangalia chanzo cha ajali ilikukomesha tatizo hilo .

“Ajalinijambo letu sisisote hatuwezi kuiachia serikali lazima tushiriki sisisote kuliondoa kabisa”.Alisisitiza Migire.

Kwaupande wake Muwakilishi  wa Wamiliki na Madereva wa Mabasi ya Mikoani (TABOA)Elimasi Emanueli amesema moja ya changamoto  wanazokumbana nazo ni sheria Mamalaka ya udhibiti na usafirishaji  Vyombo vyamoto ardhini Latra 2019 ambapo kuna mamlaka nyingine inayotoa maagizo yanayoingiliana na tasisi hiyo na kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Na Timothy Marko