KIGAMBONI YAADHIMISHA MIAKA 58 YA MUUNGANO KWA KUFANYA USAFI
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almas Nyangasa wameadhimisha siku ya muungano kwa kuungana na wananchi na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni wameshiriki usafi uliyofanyika katika viwanja vya hospitali ya Vijibweni
Akiongea mara baada ya zoezi hilo Mkuu wa Wilaya amesema miaka 58 si haba hivyo amewataka wananchi kujivunia na kuudumisha Muungano huu na kuilinda Amani tuliyonayo, pia amewataka kudumisha utamaduni wa usafi isiwe ni katika muungano tu amewataka kuendeleza katika maeneo yote majumbani na pia kujitokeza katika kila jumamosi ya mwisho ya mwezi ambapo Kwa wilaya ya Kigamboni usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi umekuwa ukifanyika kila mwezi.
Pamoja na hayo amewashukuru wananchi Kwa kujitokeza kwa wingi kuadhimisha maadhimisho ya muungano kwa kufanya usafi hospitalini hapo.
Nae Mstahiki Meya Mh.Ernest Mafimbo akizungumzia tukio hilo amesema amefurahishwa na utamaduni huu wa namna ya kusherehekea maadhimisho ya Muungano Kwa kufanya shughuli mbalimbali na jamii tofauti na ilivyokuwa awali amewataka wananchi kuudumisha Muungano na kuulinda.
Wakati huohuo mwakilishi wa kikosi cha jeshi la kujenga taifa aliekuwepo kwenye tukio ameushukuru uongozi wa wilaya kwa tukio hili muhimu lililowaleta wote pamoja na kufanikisha maadhimisho.
Nae mdau wa maendeleo ambae hushiriki na kudhamini matukio mbalimbali katika kuunga juhudi za Wilaya Ndg.Hussein Mtundu wa kampuni ya 5Point Real estate agent amesema wamekuwa wakivutiwa kushiriki katika matukio ya Wilaya kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo Kati ya uongozi wa Wilaya na jamii na kuahidi kudumisha ushirikiano huo.
Zoezi hili la usafi limehudhuriwa pia na Madiwani, Mkurugenzi na team yake ya menejimenti, Jeshi la kujenga taifa na wadau mbalimbali.
Sherehe za muungano kitaifa mwaka huu zimeadhimishwa jijini Dodoma, ambapo zimepewa kauli mbiu ni Uwajibikaji na Uongozi Bora
Aidha Kwa Manispaa ya Kigamboni maeneo mengine pia yameadhimisha Kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali.
Udumu muungano wa Tanzania, Kazi iendelee.










