ZITTO AITAKA SERIKALI KUTELEZA HOJA ZILIZOIBULIWA KATIKA RIPOTI YA CAG
Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali ya Kamati ya Bunge Zitto Kabwe ameitaka Serikali kutekeleza hoja zilizoibuliwa Ripoti ya CAG huku akibanisha kuwa Ripoti hiyo ni Mbaya zaidi ikilinganishwa na Ripoti za awali zilizotolewa na ofisi hiyo ya Mkaguzi.
Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Policy Forums Zitto Kabwe amehoji kutokuwa na uwajibikaji wa kisiasa.
"Ripoti ya Mwaka CAG ya mwaka 2021 Ni mbaya hatujaona uwajibikaji". Alisema Zitto Kabwe.
Kabwe Alisema Mapendekezo ya Mkaguzi wa mahesabu ya Serikali ya Mwaka 2021 yasipofanyiwa kazi kutakuwa na Hali Mbaya ya kisiasa ya Mwaka ujao wa fedha.
Alisema Nivyema Ripoti hiyo iweze kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri ilikuweza kujadiliwa nakutafutiwa ufumbuzi.
"Katika Mabadiliko ya katiba ya Mpya lazima wakaguzi wandani waweze kupewa
mamlaka ya udhibiti hii itaimarisha udhibiti wa fedha za Serikali". Aliongeza Zitto.
Zitto alisisitiza Hali hiyo itaweza kuimarisha mifumo ya utokajiwa fedha pasipo ukaguzi wa ndani.
Naye Rais wa Mkaguzi wa Ndani Zeiya Jeza Alisema taarifa hiyo ya Mkaguzi wa mahesabu ya Serikali imeonesha Mapungufu Makubwa ambapo amesema Asilimia 13 ya fedha yamapato yaserikali yamepotea kutokana matumizi Mabaya ya kwa baadhi ya taasisi za Serikali.
Alisema kumekuwa na utofauti Mkubwa wa Ripoti ya Mwaka CAG ya 2020 na 2021 ambapo hatisafi Asilimia 70 lakini ukaguzi wa ndani hamna tatizo.
"Tatizo taasisi nyingi hazina bodi ya Ukaguzi ilikuweza kufanya kazi kwaufanisi" AlisemaZeiya Jeza.




