JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA YAELEZA FAIDA ZA SENSA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe akizungumza na Waandishi wa habari Picha na Heri Shaaban
Na Heri Shaaban (Ilala )
Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala yaeleza faida za SENSA ya Watu na Makazi kwa Wananchi wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe alisema Sensa ya Watu na Makazi ina FAIDA nyingi katika nchi yetu ikiwemo Maendeleo ya Taifa.
"Tamko letu Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi kwa Watanzania tushiriki kuhesabiwa siku ya Agosti 23 2022 mwaka huu Ili Serikali iweze kupanga malengo yake na kujua idadi ya Watanzania kwa ujumla ni lazima tuhesabiwe" alisema Msophe .
Msophe aliwataka viongozi wa Jumuiya chama na Jumuiya kuanzia ngazi ya matawi na Kata kutoa elimu kwa Wananchi kwa ajili ya siku Maalum ya Agosti 23 kila mtu atoe ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaopita nyumbani kwako siku ya kuamkia Agosti 23/2022 Ili muweze kuhesabiwa.
Msophe alisema Ili Serikali iweze kupanga malengo yake ya kipindi cha miaka mitano lazima kwanza iweze kujua Idadi ya Watanzania kwa ujumla ndio iweze kupanga bajeti mbalimbali ikiwemo za Huduma za Jamii ikiwemo sekta ya Afya ,sekta ya Elimu miundombinu .
Aidha alisema Sensa ya watu na Makazi itasaidia serikali kujuwa jinsi gani ya kuhudumia wananchi wake kutokana na idadi yao
Pia Mwenyekiti Msophe ameshauri wananchi kutokuwaficha hata watoto ambao ni walemavu ili serikali kupata idadi yao ili kujipanga jinsi ya kuwasaidia, pia sensa itasaidia serikali kusogesa mipango mbalimbali kwenye maeneo mbalimbali kama kusogeza huduma za wananchi karibu kutokana na idadi ya watu watakaopatikana katika sensa ya 2022.




