Breaking News

KATIBU MKUU WA NCCR MAGEUZI BI MARTHA CHIOMBA ATOA UFAFANUZI JUU YA TAARIFA ZA KUENGULIWA NAFASI HIYO

Katibu mkuu wa chama cha NCCR Mageuzi Bi. Martha Chiomba ametoa ufafanuzi kufatia taarifa zilizo ripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amevuliwa nafasi ya hiyo.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam katibu huyo amesema taarifa hizo sio za kweli na ndio maana yupo ofisini akiendelea na kazi za ujenzi wa chama

"Nitoe wito kwa wanachama, wapenzi na wafuasi wetu kuwa taarifa hiyo ni ya kupuuzwa kwani hata walioitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari tayali chama kimeshawavua nafasi zao tangu mei mwaka huu"

Alisema rejea taarifa ambazo tumekuwa tukizitoa na kama chama ambazo zinatokana na vikao halali ambavyo hata ofisi ya msajili kuvitambua ni kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama na kundi lake wamevuliwa nafasi zao za uongozi na kinachongojwa ni kuitwa hili kujibu mashtaka yao na wao kuweza kujitetea.

"Aliyekuwa mwenyekiti wetu tayali amevuliwa nafasi hiyo katika kikao kilichofanyika mwezi mei na barua ya mashtaka yaliopelekea kuvuliwa nafasi hiyo anayo kinachongojwa  kuiitwa kusomewa makosa yao na wao kujieleza kisha kikao kitatoa maamuzi ya mwisho kama warejeshwe katika nafasi zao ua vingnenvyo" alisema Chiomba

Aidha Bi. Chiomba amewataka kundi hilo kuacha mara moja tabia ya kupotosha na kuzua taaruki badala yake wafate katiba ya chama kwani kitendo cha wao kuendelea kutumia nembo na jina la chama ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza jijini  Dar es salaam aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma Edward Simbeye kutoka kambi inayomwunga mkono aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia alisema kuwa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilifanya kikao cha siku moja 12 Agost na kuazimia kumvua uongozi katibu mkuu wa chama hicho, bi Martha Chiomba.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kikao hicho pia kiliazimia pia  Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Zanzibar Haji Ambari Khamis kuchukuliwa hatua za kinidhamu ndani na nje ya chama kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania wakidai kuwa kiongozi huyo anadaiwa kusababisha vurugu ndani ya NCCR-Mageuzi kwa kutumia vibaya nafasi yake.

Bw Simbeye iliongeza kuwa kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 47 kati ya 81, akisema kwa mujibu wa utaratibu akidi ya kikao hicho ilitimia. Amesema katika kikao hicho wameazimia masuala 14.