PROF MKENDA MGENI RASMI MAHAFALI YA TATU YA GLOBAL EDUCATION LINK
Dar es salaam:
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Katika Mahafali ya Tatu ya Wakala wa vyuo vikuu vya nje ya nchi GLOBAL EDUCATION LINK yatakayofanyika Tarehe 21 mwezi huu Katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar esa salaam.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Global Educational Link Ltd, Bwana Abdulmalik Mollel amsema mahafali ya mwaka huu yatawahusisha wanafunzi wote wa kitanzania walio hitimu katika vyuo vikuu vya nje ya nchi.
"Sio kila wanafunzi alifanikiwa alifanikiwa kuhitimu masomo yao kufatia uwepo wa Janga la UVIKO-19 kitu kilichopelekea baadhi ya nchi zilifungua mipaka yake hivyo Baadhi ya kozi kama udaktari walikuwa wapo kwenye kipindi Cha mafunzo." Alisema bw. Mollel
Amsema Malengo ya mahafali haya ni kukutanisha wanafunzi waliomaliza katika vyuo mbambali nje ya nchi kwa pamoja waliwa na wazazi na walezi wao kusherekea Kwa pamoja wakiwa hapa nyumbani.
Aidha bwana Mollel aliongeza kwa Lengo la pili la mahafali hayo ni Kujenga daraja Kwa wanafunzi pamoja na Taasisi mbalimbali ambazo zinazotoa ajira hasusani wanapoitaji vijana walio soma nje kwa sababu waajili wengi hutuma barua za kuhitaji vijana Hawa.
"Tunategemea kuwa jumla ya wahitimu 400 watashiriki mahafali hayo kutokana na ukubwa wa ukumbi hivyo kutoweza kumudu wanafunzi wote hivyo tumechukua wanafunzi wachache" Alisema Bwana Mollel
Aidha alibainisha kuwa katika mahafali hayo wamewaalika wadau mbalimbali wakiwemo wizara ya wizara ya Elimu, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya kazi na vijana, Wizara ya Afya sambamba na wizara ya Elimu Zanzibar.




