Breaking News

SHIRIKA LA THE FOUNDATION FOR TOMORROW KUENDELEA KUSAPOTI SEKTA YA ELIMU NCHINI


Mkurugenzi wa shirika hilo Bwana Thabisani Ncube akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika kongamano la pili la kimataifa wa masuala ya elimu bora ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania Ten/Met katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Meneja Program ya mafunzo kwa walimu wa taasisi hiyo, Bwna Noah Kayanda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna shirika hilo linavyoshiki kuwezesha kupatikanaji wa elimu bora.

Dar es salaam:

Shirika la lisilo la kiserikali la The Foundation for Tomorrow litaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha inafikia adhama yake ya kuhakikisha inatoa elimu bora na inayokidhi viwango na kwa gharama nafuu kwa wanafunzi wote.

Akizungumza katika kongamano la pili la kimataifa wa masuala ya elimu bora ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania Ten / Met jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa shirika hilo Bwana Thabisan Ncube amesema shirika wakiwa kama wadau wa sekta ya elimu nchini wamekuwa wakishirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa masuala ya elimu nchini kwa kusaidia adhima ya serikali ya kutoa elimu hususani kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

Alisema kupitia programme zao mbalimbali mstari wa mbele kusaidia na hata kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi ikiwemo kuwalipia ada na mahitaji mengine ya shule kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yao ya kimaisha na kielimu.

“shirika letu linatambua jitihada za serikali ambazo imekuwa ikizichukua katika kuhakikisha inaboresha mazingira ya elimu nchini kwa kutambua hilo tumekuwa tukishiriki katika kuhakikisha adhama hiyo ya serikali inafikiwa kwa tukitoa scholarship kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuwawezesha kupata elimu bora.” Alisema Bwana Ncube.

Aidha bwana Nembe aliongeza kuwa shirika hilo ambalo makao makuu yake yapo mkoani Arusha katika miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka huu limeanza kujenga maeneo ya kijamii ya kujifunzia ambayo yatawawezesha wananchi kujifunza kusoma na kuandika kutoka ndani na nje ya jiji hilo mradi huo upo katika eneo la Usa river pia utawasaidia wanafunzi wa kitanzania kuendana pia na kasi ya ukuaji wa kidigitali ili kusaidia katika maendeleo ya Taifa.

Alisema pia taasisi hiyo katika kipindi hicho tayali imeanzisha mradi wa vituo vya kijamii vya kujifunzia pia watatoa mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kuendesha biashara kwa lengo la kuwapa fursa ya kuandaa mawazo bora ya kibiashara na jinsi ya kuziendesha hili kuwawezesha kuwainua kiuchumi

Nae Meneja Program ya mafunzo kwa walimu wa taasisi hiyo, Bwna Noah Kayanda alibainisha kuwa pia shirika hilo katika kipindi chote cha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake limekuwa likitoa mafunzo kwa viongozi wa shule katika ngazi mbalimbali ili kuhakikisha kubwa shule zao zinatoa elimu bora.

“Shirika limekuwa likiendesha program mbalimbali katika kipindi hicho tangu kuanzishwa kwake ikiwemo kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakuu wa shule za msingi na sekondari kwa lengo la kusaidia seriklai kufikia adhima yake ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora na yenye viwango kwa faida yao na taifa kwa ujumla.