Breaking News

PROF. NDALICHAKO MGENI RASMI TUZO ZA VIJANA CHIPUKIZI ZA (TEYA)

Mjumbe wa Bodi wa Shirika la Africa Youth Transformation (AYT), Bw. Paul Siniga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna tuzo hizo jijini Dar es salaam.
Saraphina Lolo (mwenye pink) kutoka Shirika la Africa Youth Transformation  akizungumza katika mkutano huo mapema leo Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Habari kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza katika mkutano huo mapema leo.

Dar ea salaam:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tuzo za Vijana chipukizi za TEYA zitakazofanyika Agosti 27, ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Waratibu wa tuzo hizo Mjumbe wa Bodi wa Shirika la Africa Youth Transformation (AYT), Bw. Paul Siniga amesema tuzo hizo zimelenga kitoa Ari na kuhamasisha vijana  kujikomboa kiuchumi na kutangaza shughuli wanazozifanya kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Alisema kupitia tuzo hizo anaamini kuwa zitasaidia kuwapa motisha vijana pamoja na kuwadilisha mtazamo wa fikra kama vijana kuonyesha kuwa wakipewa majukumu mbalimbali wasimamie wanaweza.

Bw Siniga aliongeza kuwa Shirika limekuwa likishirikisha vijana katika kampeni mbalimbali ikiwemo  ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwaelimisha vijana namna ambavyo wanaweza kutunza mazingira.

"Shirika letu pia limekuwa likitoa elimu ya afya na uzazi kwa vijana kwa lengo la kuwasaidia vijana kujitambia na wajiepushe na majanga mbalimbali yanayoweza kuwakumba," Alibainisha Bw. Siniga

Kwa upande wake, Bi. Saraphina Lelo amesema sehemu nyingi katika kipindi kirefu vijana wamekuwa sio wanufaika wa maendeleo bali mara nyingi wamekuwa watazamaji wa program na sera zinazoathiri maendeleo yao.

Alisema kupitia tuzo hizo ni sehemu ya usaidizi wa utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 zinalenga kuwafikia vijana wote walioonyesha mchango chanya katika sekta mbalimbali za kimaendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

"Kwa mwaka huu wa 2022, Tuzo za Vijana chipukizi inategemea kutoa tuzo katika kipengele 40 ambapo vijana walishindana na siku rasmi ya kilele cha sherehe itakuwa kwa siku tatu na itaanzia Agosti 25, 26 na 27 Agosti mwaka huu," Alisema Bi. Lelo

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Habari kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA), bwana Semu Mwakyanjala alisema kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya nusu ya watanzania ni vijana maana yake ni kwamba Ndio tegemeo kubwa la nchi.

Alisema wameunga mkono jitihada hizo kwa kuwa moja ya jukumu walilonalo ni kukuza Teknolojia ya Habari na Mawailiano ( Tehama) ambapo ndilo eneo wanalolipenda vijana.

Mapema Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Haki na Mtoto Save International, Bibi Besta Mulauzi alisema wanafanya shughuli zao kwa zaidi ya nchi 100 duniani ambazo zimelenga kwenye afya, elimu, haki za watoto na maeneo mengine.

Alisema huu ni mwaka wa pili wanafadhili tuzo hizo Kwa mwaka huu wa 2022, Tuzo za vijana chipukizi (TEYA) inategemea kutoa tuzo katika vipengele 40 

Aidha, walisema kuwa, Tiketi zitakuwa za aina tatu ambazo ni 15,000 ambayo ni daraja la kawaida. 50,000 daraja la biashara, na 100,000 ambayo ni daraja la juu (VIP) kwa siku ya tatu yaani Agosti 27, 2022, 

Aidha, kamati ya maandalizi ya Tuzo hizo za vijana chipukizi (TEYA) kwa niaba ya taasisi yaani Africa Youth Transformation (AYT) imetoa shukrani  za dhati kwa ushirikiano kutoka kwa Serikali, wadau wa maendeleo mbalimbali kwa makundi yao na vyombo vya habari katika kuhakikisha dhima na lengo kuu la tuzo hizo linafikiwa. 

AYT inafanya kazi kama Asasi isiyo ya Kiserikali kukuza haki za kiuchumi na kijamii, amani, pamoja na kuboresha upatikanaji rafiki wa vijana katika elimu, afya na ushirikishwaji wa jamii ili kuondokana na umaskini nchini Tanzania.

Washiriki wa Tuzo hizo ni kulingana na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Tanzania (2007) inamuelezea kijana kama Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 35. tayari vijana hao mbali mbali wanapigiwa kura mtandaoni kupitia mitandao n tovuti ya tuzo..