Breaking News

NAIBU WAZIRI KIPANGA: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA WADAU KATIKA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI

SERIKALI imesema inatambua mchango mkubwa wa Asasi za kiraia na wadau wa elimu nchini hususani katika kusaidia, kushauri na kuboresha ya Mitaala ya elimu nchini ili kuwezasha Wahitimu waweze kujiajiri na kuajiriwa.

Akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Elimu Bora (International Quality Education Conference-IQEC) unaandaliwa na Mtandao wa TEN/MET, uliofanyika jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknojia Mheshimiwa Juma Kipanga amesema asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa na wadau muhimu hasusani katika kushauri namna bora ya kuboresha mitaala ya elimu nchini.

“Serikali inatambua na inaunga mkono jihitada za wadau wa sekta ya elimu nchini katika kuhakikisha kuwa wahitimu wetu wanakidhi soko la kimataifa na kuweza kujiajili pindi wanapomaliza masomo yao”

Alisema serikali kwa upande wake imeshaanza kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa mpaka kufika Mwaka 2025 kila Mtoto wa Kitanzania Anapata Elimu Bora na inayokidhi viwango vya soko la ajira.

"Elimu hii Bora inaendana na Uboreshwaji wa Mazingira Rafiki ya Utatikanaji wa Elimu ikiwemo Miundombinu Wezeshi ya Wanafunzi ambao Wanamahitaji Maaluum". Alisema Naibu Waziri Juma Kipanga.

Katika hatua nyingine mhe. Kipanga Aliongeza kuwa Ni vyema wadau wakaendelea kujitokeza kuendelea kutoa maoni yao ambayo yatasaidia kuboresha Mitaala ya Elimu iwe inayoendana na soko la Ajira la sasa.