Breaking News

LHRC YAZINDUA RASMI MWEZI WA DEMOKRASIA KUCHANGIZA SIASA ZENYE USHINDANI NCHINI

Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimezindua rasmi maadhimisho ya mwezi wa Demokrasi ambapo katika kipindi hicho cha maadhimisho kitafanya shughuli mbalimbali kuadhimisha siku hiyo ambayo uadhimishwa kila mwaka duniani kuaanzia 1 Agosti na kuhitimiswa 15 Septemba.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga alisema katika kipindi hicho kituo kitafanya shughuli mbalimbali  za kijamii ikiwemo utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na katiba mpya.

“LHRC kimeandaa dodoso maalum la maswali ambalo litakuwa na maswali muhususi kujua mtizamo wao juu ya katiba mpya, wangependa mchakato huo uanze na lini wangependa mchakato huo ukamilike ambapo wananchi watatakiwa kujaza” Alisema wakili Henga

Alisema tayali watanzania zaidi ya 1000 tayali wameshashiriki kujaza dodoso hilo ambalo linalenga kupata tathimini yao juu ya masuala mbalimbali hususani upatikanaji wa katiba mpya pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wao kushiriki katika maswala ya kidemokrasia.

“LHRC tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995 wamekuwa mstari wa mbele kuijengea jamii yenye kutambua haki na usawa sambamba na kuwajengea uwezo, kukuza kutetea na kuchangiza mambo yanayohusu haki za binadamu na utawala bora”

Mwezi wa demokrasia itahitimishwa septemba 15 kwa kufanyika kongamano kubwa katika ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Nyerere ambapo mijadala juu ya haki za kidemokrasia la  mwaka kuu umebeba kauli mbiu ya “Kuimarisha udhibiti wa demokrasia katika majanga ya siku zijazo” ikiambatana na maadhimisho ya miaka 30 ya Siasa za ushindani tangu kurudishwa tena nchi mwaka 1992