WAKILI HENGA ATOA WITO KWA TAASISI ZA FEDHA KUSHIRIKIANA NA AZAKI NCHINI
Na Timothy Marko
Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakili Anna Henga ameziomba taasisi za kifedha nchini kuzisaidia Azaki ziweze kuekeleza majukumu yake hili kuleta tija kwa jamii.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Azaki jijini Dar es Salaam Wakili Anna Henga amesema kuwa Asasi za kirahia kwa hivi karibuni zimekuwa zikiathiriwa na janga la Uviko 19 Hali iliyopelekea kutofanya kazi zao za kuihudumia Jamii kwa ufanisi.
Alisema Hadi kufikia Mwaka huu jumla ya Azaki 8000 zimeweza kusajiliwa nchini Tanzania ambapo Mkurugenzi wa taasisi hiyo ameiomba Serikali kuratibu Sheria ya Uanzishwaji wa Asasi za kirahia.
"Serikali Bunge na Azaki za kirahia sambamba taasisi za kifedha zinatakiwa kuzichagiza Azaki ilikuweza kuleta Maendeleo ya Watu". Alisema Wakili Anna Henga.
Wakili Anna Henga Aliongeza kuwa Kwakushirikiana Azaki zote nchini wameamua kuzisaidia jamii katika kutoa Msaada wa kisheria.
"Tunaomba Serikali ipunguze Urasmu wa utendaji kazi wa Asasi za kirahia kuweza kufanya kazi kwa ufanisi". Alisisitiza Wakili Anna Henga.
Naye Mkurugenzi wa Benki ya kibiashara CRDB, Bwana Adulmajid Nsekela amezipongeza Asasi za kirahia kuwa na utayari wa kushirikina na Sekta Binafsi.
Alisema Azaki imekuwa zimekuwa mstari wa mbele kutembelea jamii na kubaini na kutatua changamoto za jamii.
"Ninatoa Rai kwa Sekta Binafsi nchi kuendelea kuzisaidia Azaki za kirahia kuweza kuleta Maendeleo". Alisema Nsekela.




