MHE. ABBAS TARIMBA AKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WAJUMBE ZAIDI YA 600
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba akifafanua jambo katika hafla ya kukabidhi Kadi za Bima ya Afya Mabalozi na Wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM jimboni kwake
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) jijini Dar es salaam mhe. Abbas Tarimba amekabidhi Kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi wa jimboni kwake.
Dar es salaam:
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) jijini Dar es salaam mhe. Abbas Tarimba amekabidhi Kadi za Bima ya Afya kwa Wajumbe zaidi ya 600 wa Chama Cha Mapinduzi wa jimboni kwake.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Kadi hizo iliyofanyika katika ukumbi wa CCM kinondoni jijini Dar es salaam amesema lengo kubwa la lililomsukuma kutoa kadi hizo ni kutokana na umuhimu wa watendaji hao na kuwasaidia kuweza kuwafanya wawe na uhakika wa matibabu pindi wanapopatwa na ugonjwa.
"Nidhahiri kwa mwitikio huu wa Wana kinondoni jambo hili wamelipokea vizuri na wanayo furaha. Viongozi wengi wakipata nafasi, husahau waliokuwa nao, si mnaona wengi, na wengine hawasaidii mpaka wapate nafasi, hivyo mimi nimepata nguvu sana kutokana na matendo mazuri ya Rais Samia," Alisema mhe Tarimba.
Alisema viongozi wanatakiwa kuwa watu wa mfano, ambapo ameeleza kuwa pamoja na figisu na changamoto nyingi ambazo amekuwa akifanyiwa hatotingishika hata siku moja.
"Nataka niwaambie hili suala la bima ya afya limeleta mazungumzo mengi sana katika makundi mbalimbali katika Kata yetu. Tulivyolianzisha wengine wakapeleka figisu figisu juu likasimamishwa, nilivyolianzisha Makumbusho wakajitokeza wengine wakasema nafanya kampeni, jamani mimi sipigiwi kura na Wajumbe na Wenyeviti wa Mashina, lakini nimeweka siasa kando nimeangalia utu. Nimeangalia katika Katiba yetu ya Chama cha Mapinduzi kiongozi wa kwanza anayetajwa ni mabalozi,"
Alisema Tarimba
Alisema Tarimba liongeza kuwa mabalozi wengi ni watu wa zima japo kwa sasa wameanza kuingia vijana, hivyo ni busara, akili, uzoefu na mazingatio kwa viongozi hao wamekuwa wakipata changamoto nyingi ikiwemo za kutatua migogoro ya wananchi hata nyakati za usiku.
Hivyo kwa kutambua umuhimu wao na kazi yao kuwa nyeti na utu uzima wao na mazingira wanayoishi ameamua kuwakabidhi kadi hizo lengo wawe na uhakika wa maisha yao.
Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhurui ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa na Wanakinondoni katika kuwaletea maendeleo na kwamba hajawasahau.
Ameongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakipata changamoto nyingi ikiwemo za kutatua migogoro ya wananchi hata nyakati za usiku.
Hivyo kutokana na kazi yao kuwa nyeti na ya muhimu na utu uzima wao na mazingira wanayoishi ameamua kuwakabidhi kadi hizo lengo wawe na uhakika wa maisha yao.


.jpg)
.jpg)


