SERIKALI, COCA COLA YAWEZESHA MAMA LISHE 360 KIUCHUMI DAR
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akikabidhi moja ya majiko 120 ya gesi kwa wawakilishi wa Mama Lishe 360 wa Mkoa wa Dar es Salaam (kulia kwake) baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Unguu Sulay
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Mama Lishe 360 (hawapo pichani) wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwakabidhi majiko 120 ya gesi na mitungi yake; meza 120; na aproni zilizoonunuliwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania Ltd kwa mama hao.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akivalishwa aproni baada ya kukabidhi majiko 120 ya gesi na mitungi yake; meza120; aproni na mwakilishi wa Mama Lishe 360 wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania. Wanaoshuhudia ni Mama Lishe hao wakiwa kwenye viwanja vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (wa kwanza kulia) akifurahi baadhi ya kukabidhi majiko ya gesi 120 na mitungi yake, meza 120 na aproni kwa Mama Lishe 360 wa Mkoa wa Dar es Salaam (waliopo pichani) baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania kwenye eneo la Kiwanja cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama Lishe baada ya kuwakabidhi mitungi ya gesi 120 kwa niaba ya Kampuni ya Coca-Cola Kwanza kwenye Viwanja vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Vicky Myao, Mkurugenzi wa NGOs wa Wizara hiyo, Dkt. Joyce Nyoni, Mkuu wa Taasisi hiyo na Unguu Sulay, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo.
Na Mwandishi Wetu, WMJJWM, DSM
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania Ltd imewezesha Mama Lishe 360 kiuchumi wa kutoka Wilaya ya Ilala, Ubungo na Kinondoni zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) amekabidhi majiko ya gesi 120, madawati 120 yenye uwezo wa kubeba wateja 480, mitungi 120 ya gesi na kila mmoja una kilo 15, na aproni moja kwa kila Mama Lishe kwa Mama Lishe 360 wanaotoka Wilaya ya Ubungo, Ilala na Kinondoni kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao kiuchumi kupitia Programu ya Mwanamke Shujaa inayoendeshwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania Ltd
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Unguu Sulay amesema kuwa Kampuni imenunua na kuwapatia wanawake hao vifaa hivyo pamoja na mafunzo ya kutunza taarifa, kumbu kumbu, biashara na ya kisaikolojia ili kuwajengea uwezo wa kuendesha biashara kwa manufaa ya maisha ya familia zao na kuchochea uchumi wa taifa kwa ujumla kwa kutambua kuwa mwanamke ni mzalishaji na hata akipokea kitu kidogo anafanya mambo makubwa
Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Wizara hii ya makundi maalum kwa kuwa Wizara hii ni Wizara ya kitaifa na inahusu Baba, Mama, Watoto, Wajane na Makundi Maalum ambapo Mama Lishe ni sehemu ya Wizara hii na ni jicho la jamii kwa kuwa wanahudumia makundi mbali mbali ya wananchi na ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii na Serikali inatambua na kuenzi kazi ya Mama Lishe kwa kuwa anachangia uchumi wa taifa na minyororo mingine
Ameongeza kuwa Serikali itafanya tathmini na ufuatiliaji wa vifaa vilivyotolewa ili viweze kuwa na matokeo na mchango mkubwa kwenye maisha ya Mama Lishe hao ambapo ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuhudumia makundi maalum ikiwemo wanawake ambapo amepongeza Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni kwa niaba ya Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni hiyo na ameilekeza Taasisi hiyo kuunganisha wanachuo na wadau ili kuleta suluhisho la matatizo ya wananchi
Akizungumza kwa niaba ya Mama Lishe hao, Grace Victor, Mama Lishe wa Soko la Feri, Kigamboni lililopo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam ameshukuru kwa kupatiwa vifaa hivyo na atatoka kupika kwenye mkaa hadi kwenye gesi hivyo atapika kwa haraka na kupitia mafunzo waliyopewa wameelimishwa jinsi ya kulinda mtaji, kuepuka kuwa na mikopo mingi na kujitambua kuwa wanawake wanaweza na ni mashujaa
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.








