Breaking News

WAUMINI KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI KUSHIRIKI MATEMBEZI YA KUMPONGEZA MTUMISHI DKT. GEORDIE

Waumini kutoka madhehebu mbalimbali leo wamejumuika pamoja na kutoa pongenzi kwa nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo la Upako, Dokta Geodavie Kwa jinsi ambayo amekuwa akitoa misaada na kugusa jamii yote bila kujali imani zao.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mchungaji wa Taifa, Komando Mashimo amesema lengo la waumini hao kukutana ni kutoa pongezi kwa kiongozi huyo kwa jinsi ambavyo  amekuwa akisaidia na kugusa jamii bila kuangalia imani zao.

"Leo tupo hapa kutoa pongezi kwa mchungaji kiongozi wa kanisa la Ngurumo la Upako Dokta Geodavie Kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele kutoa msaada na kusaidia walio na uhitaji bila kujali imani zao, kabila na hata uwezo wao" Alisema Mchungaji mashimo.

Alisema bila kujali imani zetu tumeungana pamoja kumpongeza mchungaji Dkt. Geodavie kwani kazi anayofanya ni kubwa na ya kupongewa na kila mtu bila kujali ni kabila gani au anatokea dhehebu gani.

Mchungaji mashimo aliongeza kuwa kwa kutambua mchango wake tayali wameratibu kufanya matembezi ya kumshukuru na kumpongeza ambayo yatafanyika jijini Arusha siku ya 1 octoba kutakuwa na mbio za kilometa 5 na 10, Waimbaji wa nyimbo za injili na bongo fleva pamoja na kutoa Tuzo kwa msanii Harmonize.

Kwa upande wake sheikh  Abdul Ally amesema wao kwa mujibu wa mafundisho wamefundishwa kupenda wengine ndio maana leo unatuona tupo hapa na wenzetu kutoa pongezi kwa kiongozi huyu kufatia jinsi ambavyo amekuwa akigusa na kusaidia watu wenye uhitaji bila kujali imani zao.

"Kumekuwepo na madhebu mengi tu ya dini bayo yanatoa huduma zake miaka mingi ila mtumishi Dkt. .. amekuwa wa kitu ambacho wengi wamekuwa hawana hasa jinsi ambavyo amekuwa akitoa misaada kwa jamii bila kujali dhehebu yao" Alisema Sheikh Abdul

Katika hatua nyingine wamekemea tabia ambayo wamedai imekuwa ikishamili katika siku za hivi karibuni ya kuwakashifu viongozi wa dini hasa katika mitandao ya kijamii.

"Kumekuwepo na tabia ambayo imekuwa ikishika kasi katika siku za hivi Karibuni ya kuwatukana na kuwakashifu viongozi wa dini tunapemda kutoa rai kwa jamii kuacha mara moja kwani viongozi hao ni mmoja ya watu muhumu sana katika jamii"