Breaking News

AIRTEL TANZANIA, JUBILEE INSURANCE NA EXIEVA WAZINDUA HUDUMA MPYA YA BIMA YA AFYA. WAZIRI NAPE AELEZA MKAKATI WA SERIKALI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye Akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya gharama nafuu ambayo inayotarajiwa kuhudumia watu zaidi ya milioni 17.5 ambayo inaratibiwa kwa ushirkiano kati ya kampuni ya bima ya Jubilee, Airtel na Axieva jikini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya gharama nafuu ambayo inayotarajiwa kuhudumia watu zaidi ya milioni 17.5 ambayo inaratibiwa kwa ushirkiano kati ya kampuni ya bima ya Jubilee, Airtel na Axieva jikini Dar es salaam.

Dar es salaam
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema serikali imewekeza miundombinu na vifaa vya kisasa katika vituo vya afya kwa lengo la kuhakikisha inakuwa ili kurahisisha huduma ya afya kwa wananchi hususani wenye kipato cha chini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya gharama nafuu ambayo inayotarajiwa kuhudumia watu zaidi ya milioni 17.5 ambayo inaratibiwa kwa ushirkiano kati ya kampuni ya bima ya Jubilee, Airtel na Axieva

Amesema serikali ipo tayari kumuunga mkono mtu yeyote atakayetumia teknolojia kuokoa maisha ya watu hususani wanyonge.

“katika kuhakikisha kila Mtanzania hususani wa kipato cha chini ananufaika na maendeleo yanayotendwa na serikali, kila mmoja aone namna ya kutumia teknolojia, natamani kuona jinsi Tehama ikitumika kuokoa maisha ya watu na itakavyobadilisha maisha yao hususani katika huduma za afya,” Alisema Mhe. Nape.

Alisema watu wengi wakiwekeza kwenye afya kupitia teknolojia watasaidia kutoa mchango kwa Wizara ya Afya na kuokoa fedha nyingi za matibabu ndio maana hata serikali imelenga kwa kila Mtanzania kupata bima ya afya kwa gharama nafuu.

Aidha aliiupongeza uongozi wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bima ya Jubilee na kampuni ya Tehama. ya Axieva kwa kuanzisha bidhaa mpya ya Afya Bima ambayo ni nafuu kwa wateja wa Airtel Tanzania.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Jubilee, Dokta Harold Andamson amesema bima hiyo itakuwa ya gharama nafuu na kila mtanzania ataweza kuitumia mara tu atakapolipa kupitia Airtel Money.

Amesema bima hiyo itatumika kwa zaidi ya vituo 642 ambavyo vya serikali lengo likiwa kuwafikia watu wenye kipato cha chini kuweza kunufaika na bima hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba amesema ushirikiano wa kampuni hizo tatu ni mkakati uliolenga kuleta mapinduzi katika mazingira ya bima ya afya kwa kutoa huduma nafuu zinazoendana na soko ambazo upatikanaji wake ni rahisi kwa Watanzania wote.