Breaking News

TFS KILELENI KILIMANJARO MAADHIMISHO MIAKA 62 YA UHURU WA TANGANYIKA

Moshi.
Wahifadhi Kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania - TFS  waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa siku sita kwa ajili ya kupandisha bendera katika kilele cha mlima huo kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika wamerejea huku wanne kati ya watano waliopanda wakifika katika kilele cha mlima huo.

Wahifadhi hao walianza kupanda mlima huo Disemba 5 mwaka huu kupitia lango la Marangu ambapo pamoja nao wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali na Sekta Binafsi wakiwemo waandishi wa habari pamoja na mashirika mbalimbali walifanikiwa kupanda
mlima huo kwa ajili ya zoezi la kusheherekea miaka 62 ya uhuru kwa kuweka Bendeza ya Tanzania lakini pia Bendera ya TFS katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza mara baada ya kushuka kiongozi wa msafara huo kutoka TFS, Mhifadhi Lilian Malisa amesema TFS wahifadhi wanne kutoka TFS walifanikia kufika kilele cha Uhuru ambapo walifanikiwa kupandisha bendera ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine lakini pia walipeperusha Bendera ya TFS katika kilele hicho.

"Jana tulifanikiwa kuweka bendera ya Taifa na kupeperusha Bendera ya TFS ikiwa na ujumbe maaalum wa usichome moto katika kilele cha mlima Kilimanjaro, wahifadhi  wanne tulifanikiwa kufika kilele cha
Uhuru baada ya mmoja wetu kuugua ghafla akiwa katika Safari ya kuelekea kileleni kupitia lango la Marangu," anasema.

Alieataja wahifadhi walioshiriki kuwa ni yeye mwenyewe Lilian Malisa, Jesca Moshi Mgata, Ismaili Athumani Ndege, Nkwimba Maige Cabandour na Kiriba Maendeleo Yohana ambapo kati yao Nkwimba Maige pekee hakuweza kufika kileleni baada ya kuuguwa akiwa safarini kuelekea kileleni.