Breaking News

DCPC YATOA MSAADA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Kutoka kulia, Katibu Mkuu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es salaam DCPC Fatuma Jalala na Naibu Katibu Mkuu (katikati) Chalila Kibuda wakimkabidhi msaada wa mavazi na chakula kwa msimamizi wa  kituo cha watoto yatima cha Umra, Bi. Rahma Kishimba kilichopo Magomeni, Mwembechai jijini Dar es salaam. 

Na Mwandishi Wetu
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kimetoa msaada kwa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Umra kilichopo Mwembechai jijini Dar es Salaam.

Msaada huo ni vyakula, Sabuni, Sukari, Nguo pamoja na viatu vitu ambavyo vimetolewa na waandishi wa habari wa chama hicho.

Akizungumza Mara baada ya kukabidhi kwa Niaba ya Kamati ya Utendaji na Wanachama wa DCPC jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Bi. Fatuma Jalala amesema waandishi ni sehemu ya jamii hivyo wanawajibika kwa jamii hasa kwa kuangalia makundi yenye uhitaji ikiwemo kutuo cha Umra

Amesema msaada huo ni mwanzo wa kuendelea kutoa msaada katika makundi mengine chama kupitia wanachama kimejipanga kuendelea kufanikisha utoaji wa msaada huo.

Aidha amesema wanachama ndio nguzo inayoshikilia kufanikisha majukumu mbalimbali na kuwataka wasichike kutoa misaada pale panapohitajika.

Bi.Fatuma aliongeza kuwa waandishi wamekuwa sehemu ya kuandika wengine wanaotoa msaada lakini sasa ni tofauti sisi wenyewe kusaidia jamii.

Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Umra Rahma Kishimba ameshukuru DCPC na kuwaomba waendelee kuwangalia kwa mara nyingine kutokana na mahitaji ya kituo hicho.

Amesema licha ya DCPC kujitoa ameomba Taasisi zingine kuiga mfano wa DCPC katika kusaidia makundi yenye uhitaji.

"Nimefarijika sana waandishi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika Umra hiyo ni mipango ya Mungu" Amesema Kishimba"

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es salaam (DCPC) wakiwa katika pucha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada kwa msimamizi wa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Umra Magomeni, Mwembechai jijini Dar es Salaam.