Breaking News

MKOMBOZI BANK YAZINDUA JENGO JIPYA LA TAWI MT. YOSEPH NA MAKAO MAKUU YAKE JIJINI DAR

Baba Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es salaam Jude Ruwai’chi akiwa na picha ya pamoja na watendaji kutoka benki ya Mkombozi katika hafla ya hafla ya uzinduzi wa jengo jipya na tawi na makao makuu ya benki jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Imeelezwa kuwa kutokuwa na uelewa juu ya matumizi ya mikopo kwa watanzania wengi ni moja ya changamoto kubwa kwani wengi wamekua wakikopa kisha kutumia mikopo hiyo kufanya shughuli nyingine nje ya biashara husika.

Akizungumza Jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya na tawi la Mt.  Yoseph na makao makuu ya benki ya Mkombozi, Baba Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es salaam Jude Ruwai’chi amesema miongoni mwa mikopo inayofifisha maendeleo ni pamoja na kausha damu.

Amesema watanzania wanapaswa kuomba mikopo katika taasisi za kibenki pamoja na kuheshimu dhamira ya mikopo hiyo huku akitumia nafasi hiyo kuwashahuri wanaokopa kujikita katika biashara.

"Napenda kutoa rai kwa wananchi kuomba mikopo katika taasisi za kibenki pamoja na kutumia mikopo hoyo kwa mujibu wa malengo yake" Alisema Askofu Ruwai’chi

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji benki ya Mkombozi, bwana Respite Kimati amesema tayari benki hiyo imejipanga kuanza kutumia nyenzo za kisasa za teknolojia katika kufikisha huduma za kibenki kwa watanzania hususani maeneo ya vijijini.

Alisema katika kuhakikisha malengo ya benki hiyo yanafanikiwa tayari benki hiyo imeanzisha huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya  (MKOMBOZI WAKALA) ambayo ina zaidi ya mawakala mia saba (700) katika maeneo mbalimbali nchini,  huduma za kibenki kwa mtandao (internet Banking), hutoaji wa huduma kwa njia ya simu (Mkombozi Mobile) kupitia ujumbe mfupi wa maneno (USSD Code) pamoja na Aplication.

Aidha bwana Kimati ameongeza kuwa benki hiyo pia katika kuhakikisha inasongeza karibu zaidi huduma zake kwa wateja wake tayali ina jumla ya matawi kumi na tatu, ambapo mkoa wa Dar es salaam ukiwa na matawi manne, ikifatiwa na Meanza yenye matawi mawili, Arusha, Moshi, Morogoro, Bukoba, Iringa na Njombe.

Alisema kwa kuzingatia mahitaji ya soko tayali benki hiyo imeanzisha huduma ya kukusanya mapato katika taasisi za kidini (SADAKA Digital) pia ipo mbioni kuanzisha  na kuleta somoni huduma zingine mahusisi katika huduma kama vile mashileni na mahospitalini.

Alibainisha kuwa kupitia kupitia dira yake benki hiyo itaendelea kujikita katika kutoa huduma zote za kiuchumi hususani kwa wateja wadogowadogo kwa kuzingatia hali inayoyazinguka makundi haya.

Uzinduzi wa Jengo jipya la tawi la Mt. Yoseph na makao makuu ya benki umehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo wajumbe wa bodi. pia benki hiyo ilitumia wasaa huo kubainisha mikakati yake kwa makundi mbalimbali ya biashara na hutoaji wa huduma pamoja na kujenga uwezo endelevu wa kulipia gawio kwa wanahisa wao.