PURA NA ZPRA WAJADILIANA NAMNA BORA YA KUBORESHA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA ASILIA NCHINI
Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni akifafanua wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Alfan Alfan akizungumza na waandishi mara baada ya mkutano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji ZPRA Adam Makame akizungumza na waandishi mara baada ya mkutano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi Taasisi ya Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar (ZPRA) Ali Mirza akizungumza na waandishi mara baada ya mkutano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) jijini Dar es Salaam.
Dar es salaam:
Watendaji wa wakuu wa Bodi za Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) pamoja na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) wamekutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kujadilia namna bora kuboresha sekta Mafuta na Gesi asilia nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Mkutano Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni amesema kikao kazi hicho kimezikuta isha mamlaka hizo kwa lengo la kujadiliana namna bora kuboresha sekta ya Mafuta na Gesi asilia nchini.
"Katika kikao chetu cha leo lengo kubwa ni kujadilina pamoja na kubadilishana uzoefu ili tuweze kudhibiti na kuendeleza sekta hii muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu, tunatumaini baada ya kikao hiki tutaainisha mikakati yetu na kuifanyia kazi ipasavyo" Alisema Mhandisi Sangweni.
Alisema katika kikao hicho pia wameweza kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuifanya sekta hiyo kuweza kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji ZPRA, bwana Adam Makame amesema lengo la mkutano huo ni kujadilia namna kuweka mazingira bora kwa pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji.
"Tumekutana kwa lengo la kushauliana juu ya namna bora ambavyo tunaweza kupanga mipango na mikakati ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia hili iwezesha kutoa mchango kwa taifa letu" Alisema Bw Makame.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya PURA, bwana Alfan Alfan amesema ushirikiano wa PURA na ZPRA umelenga kujenga mahusiano ya muda mrefu katika kuhakikisha kuwa wanahamasisha na kutangaza fursa hiyo hili kuwavutia wawekezaji Tanzania Bara na Visiwani .
"Ushirikiano kati ya PURA na ZPRA ni chachu ya Kutangaza vitalu vyetu nakupata wawekezaji wengi hivyo sekta ya Mafuta na Gesi asili itazidi kukua nakuleta maendeleo kwa Taifa letu" Alisema Bw. Alfan.







