CUF YAADHIMISHA MIAKA 23 YA VIFO VYA WANACHAMA WAO MWAKA 2000, WASISITIZA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Chama Cha Wananchi (CUF), leo January 27 kimeazimisha kumbukumbu ya miaka 23 ya mauaji ya wanachama wa chama hicho yaliotokea Unguja na Pemba kisiwani Zanzibar kufatia maandamano ya amani yaliyofanyika kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 kutokuwa huru na haki
Akizungumza makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema maandamano hayo ya amani ambayo yalikuwa na lengo la kuitaka serikali kutekeleza maoni ya waangalizi wa uchaguzi kuwa haukuwa wa huru na haki hivyo kutaka uchaguzi huo urudiwe kwa kufuata Katiba, Demokrasia Utawala Bora.
"Uongozi wa chama uliamua kuanzisha maandamano ya amani nchi nzima kuitaka na serikali kutekeleza maoni ya waangalizi wa uchaguzi waliotoa ripoti ya uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki hivyo kudai Katiba yenye Demokrasia Utawala Bora unaoheshimu haki za watu" Alisema Prof. Lipumba.
Alisema pamoja na jitihada zote ambazo wadau wa vyama vya siasa wamekuwa wakizichuchukua kwa lengo la kuweka mazingira bora na uchaguzi hususani swala la mchakato wa katiba mpya kutokuzaa matunda hadi sasa tunapoadhimisha 23 bado uchaguzi kutokuwa huru na wa haki.
Aidha Prof. Lipumba amesema zimekuwepo jithada mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa khadhia hiyo aijirudii tena wao kama chama walitoa mapendekezo kwa serikali kama mchakato wa Katiba hautakamilika yafanyike Mabadiliko madogo ya sheria ikiwemo uwepo Tume huru ya uchaguzi, mgombea binafsi pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Rais kupingwa mahakamani.
“Katika Mkutano wa Baraza la Vyama tuliokutana Dodoma mambo yaliyojitokeza ya wazi kabisa ni kwamba pana kila sababu ya kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya, kuna umuhimu wa kuweza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, baadaye Rais akaunda Kikosi Kazi lakini mapendekezo ya wazi yashatoka kwenye Mkutano na walikuwepo Viongozi wa Serikali 15 Desemba 17 2021 hivyo nisisitiza kwamba muda uliokuwepo kama pana utashi wa Kisiasa kushughulikia mambo haya” ALisema Prof. Lipumba na kuongeza kuwa,
“Agosti 2023 TCD (Kituo cha Demokrasia Nchini) kiliitisha Mkutano wa Wadau kutazama hali ya Kisiasa kuelekea kwenye Uchaguzi wa mwaka 2024 na mwaka 2025 katika maadhimio ya TCD yaliyotolewa moja ilikuwa ni kwamba suala zima la mchakato wa kupata Katiba Mpya likwamuliwe tuweze kupata Katiba Mpya, na tukatilia shaka huenda mabadiliko ya Katiba kwa ujumla yanaweza yasikamilike kabla ya Chaguzi wa 2024 na 2025 hivyo tukatoa mapendekezo Serikalini kwamba yafanyike mabadiliko madogo ya Katiba ili kuruhusu Chaguzi za Kidemokrasia”
Sambamba na hayo amesema Mabadiliko hayo yafanane na yale ambayo wanachama Vyama vya TCD walikubaliana na Rais Kikwete mwaka 2014 kwamba kwakuwa mchakato wa Katiba hautakamilika basi angalau mabadiliko madogo ya Katiba yafanyike, ambayo ni pamoja na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, mgombea binafsi, Rais atangazwe ameshinda ikiwa atapata Kura halali zilizopigwa asilimia 50 + 1 na Uchaguzi wa Rais uhojiwe Mahakamani.
Alisema kwa sasa kama kweli serikali ina nia njema walau kuepuka ambayo yakijitokeza kwenye uchaguzi huko nyuma mfano mwaka 2019/2020 Watu wenye sifa waombe nafasi ya kuwa wajumbe na kupita kwenye usaili na Tume iwe na watendaji wake walau Hadi nafasi ya Jimbo.
Akizungumzia juu ya miswada mitatu iliwasilishwa bungeni ametoa wito kwa Mihimili miwili ya Dola Nchini (Serikali na Bunge) kutumia njia bora itakayofanikisha kufanyika kwa mabadiliko madogo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ili kuruhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu (2024) na Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwakani (2025) uwe Huru na Haki
"Miswada mitatu iliyowasilishwa na Serikali Bungeni mwishoni mwa mwaka Jana (2023) haina tija na kwamba haijajibu mahitaji halisi yanayopigiwa kelele kwa miaka mingi na Wadau wa Siasa na Demokrasia Nchini" Alisema Prof. Lipumba




