KIKAO CHA KAMATI KUU ACT WAZALENDO KUFANYIKA LEO JAN 27 JIJINI DAR
TAARIFA KWA UMMA
YAH: KIKAO CHA KAMATI KUU
Chama cha ACT Wazalendo kitafanya kikao cha Kamati Kuu kujadili masuala mbalimbali ya Ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla. Pamoja na Mambo mengine Kikao hicho kitateua Makatibu wa Majimbo na Mikoa Tanzania Bara na Zanzibar, Itapitia Taarifa ya Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya Chama, Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Taifa utakaochagua viongozi wa chama ngazi ya Taifa utakaofanyika mwezi Machi, 2024, Hali ya Kisiasa nchini nk.
Kikao hicho kitafanyika leo Tarehe 27/01/2024 katika Ukumbi wa Juma Duni Haji uliopo Ofisi za Makao Makuu Magomeni - Usalama Dar es Salaam.
Pamoja na Salaam za chama, tunatanguliza shukrani.
Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu Katibu Habari Uenezi na Mahusiano na Umma
Leo Tarehe 27/01/2024.




