Breaking News

DKT. ANANILEA NKYA AITAKA NGOME YA WANAWAKE ACT WAZALENDO KUPINGA VITI MAALUMU

Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu WA Ngome ya Wanawake ya Chama cha ACT wazalendo Dkt. Ananilea Nkya akizindua Sera ya Jinsia ya Chama cha ACT Wazalendo. Sera ya Jinsia ya ACT inaweka msingi na masharti ya kuwa na usawa wa kijinsia katika uongozi ndani ya ACTwazalendo katika mkutano mkuu wa ngome ya wanawake ya chama, uliofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 2, 2024

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba na Sheria (JUKATA), Dkt. Ananilea Nkya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo mkutano ambao ulienda sambamba na kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa ngome hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo jijini Dar es Salaam, Machi 2, 2024
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Dorothy Semu akifafanua jambo katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo mkutano ambao ulienda sambamba na kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa ngome hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo jijini Dar es Salaam, Machi 2, 2024.

Dar es Salaam:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba na Sheria (JUKATA), Dkt. Ananilea Nkya ameitaka Ngome ya wanawake ya ACT Wazalendo kujipanga na kujitokeza kuunga mkono hoja ya kuondelewa kwa nafasi ya Viti Maalum Bungeni ili kuisaidia Serikali kupungua gharama hili fedha hizo kuweza kufanya mambo mengine ya maendeleo kama kutatua kero za wananchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo Machi 2, 2024 jijini Dar es Salaam ambao ulienda sambamba na kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa ngome hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika ukumbi wa haikande makao makuu ya chama hicho.

“Napenda kutoa rai Tuwe mstari wa mbele kunapendekeza mfumo wa viti maalumu ufutwe ili kila mwanamke aende majimboni kugombea na nyinyi Ngome ya Wanawake ACT, pambaneni na kulisemea hili ili mkakati huu ufanikiwe jambo litakalosaidia Serikali, fedha zinazotumika kwa ajili ya kulipa wabunge ambao hawana majimbo zikafanye kazi nyingine za kijamii,” Aliesema Dkt. Nkya na kuongeza kuwa 

“Mheshimiwa Rais wetu ni msikivu na mkilisema hili na akalisikia, naamini anaweza kufanya mabadiliko katika jambo hilo, pazeni sauti ili kulifikisha suala hilo kwa Rais wetu mpendwa, sina shaka atalisikia tu na atafanya maamuzi,”

Alisema zaidi ya shilingi 300 zimekuwa zikitumika kulipa wabunge hao wa viti maalum hivyo ni vema jambo hilo likapigiwa kelele ili kuokoa fedha hizo ambazo kimsingi zinaweza kufanya mambo makubwa kwa ajili ya wananchi kwa kuwaletea maendeleo pamoja na kutatua changamoto zao.

Aidha Dkt. Nkya pia ameitaka Ngome ya Wanawake ya chama hicho kuendelea kushawishi Kamati Kuu ya chama hicho kutoa nafasi nyingi kwa wanawake hasa kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani katika uchuguzi mkuu.

Alisema wajumbe wa mkutano huu kuwa makini katika kuchagua viongozi wa ngome hiyo kutokanana kutoa viongozi wanawake ambao wanakuja kufanya vizuri katika chaguzi ikiwemo nafasi ya urais kama ilivyokuwa mwaka 2015.

Katika hatua nyingne Dkt. Nkya emeelezea juu ya umuhimu wa katiba alisema wakati Tanzania inaingia katika mfumo wa vyama vingi ilitakiwa pia kubadilishwa na katiba ili kutoa nafasi ya kuingizwa mfumo wa vyama vingi jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa changamoto nyingi nyakati za uchaguzi.

"Kutokana kuendelea kuwepo na changamoto nyingi nyakati za uchaguzi kutokana mapungufu yaliopo katika katika ya sasa bitoe rai kwa ngome ya wanawake kupigania kupatikana kwa Katiba Mpya ili kutoa fursa ya kufanyika kwa mabadiliko yanayohitajika ili kukidhi mfumo wa vyama vingi kufanya vizuri"Alisema Dkt. Nkya


Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (JUKATA), Ananilea Nkya (hayupo pichani) katika mkutano mkuu wa ngome ya wanawake ya chama, uliofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 2, 2024
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Dorothy Semu (wa nne kushoto) Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (JUKAT), Ananilea Mkya (wa tano kulia), viongozi wengine wa chama, wageni waalikwa na wajumbe wa ngome ya wanawake wa ACT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa ngome hiyo, uliofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 2, 2024.