Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 4, 2024 ameongoza matembezi ya kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ill kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo ya kilomita 10 yalianzia Coco Beach jijini Dar es salaam hadi mzunguko wa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam na kurudu Coco Beach.