TWANGA PEPETA, FM ACADEMIA, MALAIKA BAND JUKWAA MOJA KATIKA TAMASHA LA GRAND GALA DANCE
Tamasha kubwa la Grand Gala Dance awamu ya tatu kufanyika siku ya AGOUST 30 katika ukumbi wa Super Doom masaki.
Akizungumza juu ya maandalizi ya tamasha hilo mkuru6wa Chocolate princess limited, Bi Mboni Bisimba amesema mwaka huu tanasha hilo limeboreshwa zaidi ukilinganishwa na yaliopita ambapo mwaka huu bendi kubwa za Fm ACADEMIA, Twanga Pepeta na Malaika band chini ya uongozi wa Christian Bela.
"Msimu huu wa tatu wa tamasha la GRAND GALA DANCE umeboreshwa zaidi kuanzia katika burudani nzuri pamoja ambazo itatolewa na band kubwa nchini katika jukwaa moja" Alisema Bi Mboni Bisimba
Alisema katika kuhakikisha kuwa mwaka huu tamasha hilo linafana zaidi wadhamini wakuu wa tamasha hilo bank ya CRDB wamejipanga kuhakikisha kuwa kila mpenzi na shabiki wa mziki wa dance anapata burudani kwa viwango vya hali ya juu.
Akizungumzia kuhusu viingilio siku ya tamasha hilo ambavyo vitafanyika kupitia lipa namba ya CRDB, TEMBO Card amesema kutakuwa na viingilio vya aina tatu ambavyo ni VVIP milioni 2, VIP laki moja pamoja na shilingi 50 kwa mtu mmoja.
Mapema akizungumzia juu ya maandalizi ya band ya FM ACADEMIA , Pachko Mwamba amesema wamejipanga kuhakikisha luwa wanako moyo ya mashabiki wa mziki wa dansi nchini na kuwataka kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushuhudia buridani kali kugoka kwa band hiyo.
"Sisi kama FM ACADEMIA wazee wa Ngwasuma tumejipanga kuhakikisha kuwa siku hiyo tunatoa burudani kwa wapenzi wa mziki wa Dance kuhakikisha kuwa wanakata kiu yao kwa kutoa show kali" Alisema Pachko Mwamba
Tamasha la Grand Gala Dance msimu wa tatu mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Damas Ndumbaro akimwakilisha waziri mkuu Kasimu Majaliwa.




