ACT TUPO TAYALI KUWATUMIKIA WANANCHI NA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO
Dar es salaam - Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Bi Dorothy Semu amesema katika kipindi cha miaka 11 tangu kuasisiwa kwa chama hicho kimejipambanu kama moja ya chama ambacho kimejikita zaidi katika kuwasemea Wananchi juu ya changamoto zao pamoja kutoa suluhisho la kuzitatua.
Akizungumza mapema leo Mei 05, 2025 katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuasisiwa kwa chama hicho zilizofanyika nakao makuu ya chama Magomeni katika ukumbi wa Mikutano wa Hakainde Hichilema jijini Dar es salaam.
"ACT katika miaka yote 11 tangu kuasisiwa kwake kmekua ndio chama kilichojikita kujenga jukwaa mbadala ambalo ni kimbilio kwa wanasiasa wote ambao wanapenda siasa safi na ambao hawaridhishwi na ukandamizaji wa Demokrasia kwenye vyama vyao vya Siasa". Alisema Bi Semu.
Alisema moja yq kielekezo Cha mafanikio yao makunwa ni kumpokea marehemu Maalim Seif Hamad na Wenzake mwaka 2019 hii inatokana na kuaminika kwa Chama hiki na jabari la Siasa kwa afrika mashabiki na Duniani kwa ujumla.
"Chama kimekuwa kikitoa nafasi kwa vijana na tumeendelea kuwapa nafasi vijana kuonyesha Uwezo wao kwenye Uongozi na Mfano mkubwa ni kumchagua katibu Mkuu wa Chama hiki akiwa na miaka 34 hii ni alama ya wazi kwa vijana wote kuwa Chama Cha ACT wazalendo ndio Jukwaa lao". Alisema Bi Semu.
Aliongeza kuwa Chama kimejenga jukwaa la wanawake sambamba na kuvunja minyororo kandamizi kwa demokrasia na kuonyesha kwa vitendo juu ya dhana ya usawa wa jinsia kwa kuhakikisha kuwa Kuna usawa wa kijinsia kwenye vyombo vyote vya maamuzi.
"ACT pekee ndio Chama ambacho unaweza kukuta nafasi za kwenye chombo Cha maamuzi Halmashauri kuu, Kamati kuu uchaguzi umefanyika kwa mfumo 50 kwa 50". Alisema Bi Sema.
Chama cha ACT Wazalendo leo Mei 5, 2025 kimetimiza Miaka 11 tangu kuanzishwa kwake na kinajivuni mafanikio makubwa.






