ALIYEPOSTI' SIKU ZA KITΙΜΑ ZINAHESABIKA AKAMATWA
Dar es salaam - Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limemkamata Frey s/o Edward Cossey ( 51 ) Mkazi wa Dodoma na Mbezi beach Makonde Dar es Salaam kufuatia
chapisho lake la vitisho dhidi ya Padri Charles Kitima alilolitoa kwenye mitandao ya kijamii siku chache kabla ya tukio.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 5, 2025 Jijjini Dar es Salaam, Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne Muliro
amesema wanaendelea na mahojiano na upelelezi wa shauri hilo unaendelea
Aidha, Kamanda SACP Muliro amesema Mei 3, 2025 maeneo ya Kibada Kigamboni
Dar es salaam walikamatwa watu watano wakihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi gunia 60 zilizokuwa zimepakiwa kwenye gari no T 466 EDV aina ya HOWO lenye tank namba T 994 EEG.
Watuhumiwa hao na Nathan s/o Danga maarufu kama masumbulo, Ali s/o Musa, Abdala s/o Athuman, Mohamed s/o Chahama na Upendo d/o Mgonja watafikishwa kwenye vyombo vya Sheria
Hata hiivyo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata David s/o Zefania Snga (39) mfanyakazi wa bima wa zamani wa kampuni ya UAP kwa kutoa taarifaa zaa uongo kituo cha Polisi Kigamboni kuwa kuna magari mawili namba T 811 DUL Toyota Crown na T 647 DRE Mitsubishi Outlander kuwa magari hayo vifaa vyake mbalimbali vimeibiwa.
"Polisi walivyofuatilia walibaini kuwa mtuhumiwa alikuwa ameving'oa na kuvificha nyumbani kwake kwa lengo la kujipatia pesa kwenye kampuni ya bima kwa njia ya udanganyifu",alisema Kamanda Muliro
Pia amesema kwamba vifaa vilivyong'olewa na kufichwa ni bampa za mbele na nyuma,window covers,radio za gari,side mirrors,taa zote za mbele na nyuma,power windows na betri.Jeshi la polisi linakemea vikali tabia za kutoa taarifa za uongo kwa makusudi kwa maafisa wa Serikali na halitasista kuchukua hatua za kisheria.




