WAANDISHI WA HABARI 1200 WAJISAJILI BODI YA ITHIBATI
Dar es salaam - Waandishi 1,200 wamejisajili kwenye mfumo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) mpaka jana.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula amesema kwamba leo ndiyo mwisho wa waandishi kujisajili na hakutakuwa na muda wa nyongeza.
Dirisha la usajili kwenye mfumo wa JAB lilifunguliwa mwezi uliopita na waandishi wanaojisajili wanapata vitambulisho maalumu vitakavyowawezesha kufanya shughuli za kihabari. Leo ndiyo tarehe ya mwisho ya kujisajili.
"Usipojisajili hautaruhusiwa kuchukua wala kuchakata habari, kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za kisheria ambapo adhabu yake ni faini, kifungo jela au vyote kwa pamoja," alisema Kipangula alipozungumza na gazeti la Habari leo.
Kwa mujibu wa JAB, mwandishi ambaye hatojisajili kwenye mfumo na kupatiwa kitambulisho hatoruhusiwa kuchakata habari zozote zikiwamo za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.




