Breaking News

CHINI YA RAIS SAMIA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA KIDIJITALI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 103

Idadi ya watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu nchini imeongezeka maradufu kutoka milioni 32.7 mwaka 2021 hadi milioni 66.5 mwaka 2025, sawa na ongezeko la asilimia 103.4.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), miamala ya malipo kupitia mtandao wa simu imepanda kutoka shilingi trilioni 5.06 mwaka 2023 hadi shilingi trilioni 6.41 mwaka 2024, ongezeko la asilimia 26.73.

Aidha, takwimu za International Data Centre Authority (IDCA) za mwaka 2024 zinaonesha kuwa uchumi wa kidijitali umechangia asilimia 15 ya pato la dunia, sawa na dola za Marekani trilioni 16.

Wataalamu wanasema ukuaji huu unaonyesha nafasi kubwa ya teknolojia katika kurahisisha huduma, kuongeza ajira, na kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye pato la taifa.