Breaking News

MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA LAINI ZA SIMU MILIONI 37.4 ZASAJILIWA, WATUMIAJI WA INTRANETI WAFIKIA MILIONI 20,

Zaidi ya laini mpya za simu milioni 37.4 zimesajiliwa nchini katika kipindi cha miaka minne, hali iliyopelekea idadi ya laini za mawasiliano kuongezeka kutoka milioni 53 mwaka 2021 hadi kufikia milioni 90.4 mwaka 2025, sawa na ongezeko la asilimia 70.

Wakati huo huo, watumiaji wa intaneti wameongezeka kwa zaidi ya milioni 20, kutoka milioni 29.1 mwaka 2021 hadi milioni 49.3 mwaka 2025, sawa na ongezeko la asilimia 68.

Mafanikio haya yanatajwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kidijitali wa Miaka Kumi (2024–2034) na Mkakati wa Taifa wa Brodibandi (2021–2026) ulioanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, unaolenga kuimarisha miundombinu ya TEHAMA, kurahisisha upatikanaji wa huduma, na kuongeza pato la Taifa.