Breaking News

MOROGORO KUWA MKOA WA VIWANDA – DKT. SAMIA

Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni zake za kuomba kura kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Jana, Dkt. Samia alifanya mikutano mikubwa miwili ya kampeni, asubuhi katika eneo la Ngerengere na jioni mjini Morogoro, ambapo alipokelewa na umati mkubwa wa wananchi wenye hamasa kubwa.

Katika mikutano hiyo, Dkt. Samia ameahidi kuufanya Mkoa wa Morogoro kuwa miongoni mwa mikoa ya viwanda nchini, ikiwa ni sehemu ya ajenda ya serikali ya CCM ya kukuza uchumi kupitia uwekezaji wa viwanda na kuongeza ajira.