Breaking News

NLD YAKAMILISHA ZOEZI LA KUSAKA WADHAMINI, KUREJESHA FOMU AGOST 24

Chama cha National League for Democracy (NLD) kimemaliza rasmi zoezi la upatikanaji wa wadhamini kwa ajili ya mgombea wake wa urais, Mheshimiwa Doyo Hassan Doyo, aliyekusanya wadhamini katika mikoa yote 10 ya Tanzania Bara na Visiwani.

Zoezi hilo lilianza tarehe 10 Agosti 2025, mara baada ya mgombea huyo kuchukua fomu ya uteuzi, na limehitimishwa leo 22 Agosti 2025, jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Lamada. Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, mgombea huyo ameapishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, jambo linalomwezesha kuendelea na mchakato wa kisheria wa uteuzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NLD, Doyo anatarajiwa kurejesha fomu ya uteuzi rasmi tarehe 24 Agosti 2025, jijini Dodoma, ambapo atasubiri uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Chama hicho kimeishukuru jamii kwa kujitokeza kwa wingi katika hatua hiyo, kikisisitiza kwamba kitaendelea kusimama imara kwa maslahi ya wananchi na maendeleo ya taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Don Waziri Mnyamani, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Taifa wa NLD