Breaking News

VITUO VYA AFYA ZAIDI YA 4,900 VYAUNGANISHWA NA MFUMO WA GoTHOMIS NCHINI

Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kusogeza mbele matumizi ya TEHAMA katika sekta ya afya kwa kuboresha mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya ujulikanao kama Government of Tanzania Hospital Management Information System (GoTHOMIS).

Takwimu zinaonesha kuwa hadi sasa jumla ya vituo 4,915, sawa na asilimia 67.88 ya vituo vya kutoa huduma za afya ngazi ya msingi, tayari vinatumia mfumo huo. Miongoni mwa hivyo, hospitali za halmashauri ni 186, vituo vya afya 848, zahanati 3,860, kliniki 3, hospitali teule za wilaya 7 pamoja na vituo vingine 11 vinavyomilikiwa na taasisi za umma.

GoTHOMIS umeelezwa kuwa chachu ya kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi, na kuimarisha usimamizi wa rasilimali katika sekta ya afya nchini.