AWAMU YA SITA YAUNGANISHA NCHI KUPITIA UJENZI WA MIUNDOMBINU
Chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Awamu ya Sita imeimarisha mtandao wa barabara nchini kupitia mikakati ya uwekezaji katika sekta ya miundombinu.
Takwimu zinaonyesha urefu wa barabara umeongezeka kutoka kilomita 108,946 mwaka 2020 hadi kilomita 144,430 mwaka 2025. Aidha, barabara za changarawe zimepanuka kutoka kilomita 24,493 hadi kilomita 44,372.2, huku barabara za lami mijini na vijijini zikiongezeka kutoka kilomita 2,025 hadi kilomita 3,467.3 katika kipindi hicho.
Maendeleo hayo ni matokeo ya utekelezaji wa sera na mipango madhubuti ya serikali, yenye lengo la kufungua fursa za kiuchumi, kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na bidhaa nyingine, pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wa vijijini na mijini.
Hatua hizo zimeifanya miundombinu ya barabara kuwa nguzo muhimu ya ukuaji wa uchumi na chachu ya maendeleo ya taifa.