RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMALIZA MSONGAMANO JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka mkakati kabambe wa kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya usafirishaji.
Miongoni mwa hatua kubwa zinazotekelezwa ni Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT). Awamu ya pili ya mradi huo, kutoka Mbagala hadi Kariakoo, tayari imekamilika, huku awamu ya tatu inayotoka Gongo la Mboto ikiwa imefikia asilimia 80 ya utekelezaji. Aidha, awamu ya nne kutoka Tegeta imekamilika kwa asilimia 22.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 681.5 na unalenga kutoa suluhisho endelevu la usafirishaji wa umma, kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kurahisisha huduma za usafiri kwa wananchi wa Dar es Salaam.