Breaking News

RAIS SAMIA ABORESHA SOKO LA KAKAO, BEI YAPANDA MARADUFU

Bei ya zao la kakao nchini imeongezeka maradufu katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, hatua inayodaiwa kuwa ishara ya jitihada za Serikali kuwajali wakulima kwa kuwatafutia masoko ya uhakika kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2020 bei ya kilo moja ya kakao ilikuwa shilingi 4,570, huku mwaka 2025 ikipanda hadi shilingi 19,979. Aidha, mauzo ya nje ya zao hilo yaliongezeka kutoka tani 40,000 mwaka 2020, zilizowaletea wakulima mapato ya dola za Marekani milioni 44 (sawa na shilingi bilioni 110), hadi tani 70,000 mwaka 2025, ambazo zimeingiza dola milioni 109 (takribani shilingi bilioni 290).

Kwa mujibu wa wachambuzi wa sekta ya kilimo, ongezeko hilo la bei na mauzo linaashiria mikakati ya Serikali ya Rais Samia ya kukuza thamani ya mazao ya wakulima kupitia uboreshaji wa masoko na mifumo ya biashara.

Wadau wa sekta hiyo wanasema hatua hiyo ni chachu ya kuongeza kipato cha wakulima na kuchochea maendeleo ya kiuchumi vijijini.