VIONGOZI ACT WAZALENDO WAKUTANA, WAJADILI HALI YA KISIASA NCHINI
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, ameongoza kikao cha kawaida cha Kamati ya Uongozi ya Taifa kilichojadili masuala mbalimbali, ikiwemo hali ya kisiasa nchini.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatano, Aprili 29, 2026, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya chama, Vuga, Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Mwenyekiti wa Taifa, Ndugu Othman Masoud Othman; Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Ndugu Ismail Jussa; na Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara, Ndugu Is-haka Mchinjita.
Wengine ni Katibu Mkuu wa chama, Ndugu Ado Shaibu Ado; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ndugu Omar Ali Shehe; pamoja na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Ndugu Ester Thomas
.
Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa chama, Ndugu Omar Said Shaaban, Kiongozi Mstaafu wa chama, Ndugu Zitto Zubeir Kabwe, Mwenyekiti Mstaafu, Ndugu Juma Duni Haji; pamoja na Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi, Ndugu P.R.F. Omar Fakih Hamad.
Vilevile, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Zanzibar, Ndugu Nassor Ahmed Mazrui, alikuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.








