Breaking News

JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MTOTO

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kwenda jela miaka 30 Said Hemed Matuli, 58, mkazi wa Airwing Ukonga, kwa kosa la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.mwenye umri wa miaka 15. Kesi hiyo namba CC 4710/2026 imesikilizwa mbele ya Hakimu Aneth Nyenyema. 

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mhanga wa tukio hilo ni mkazi wa Kitunda, kwa mujibu wa mashtaka, mtuhumiwa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na binti huyo mnamno tarehe kati ya mwezi Julai 2025.

Inadaiwa walikutana wakati mhanga akiwa anafanya biashara ya kutembeza mboga mboga siku za wikendi. Mahusiano hayo yaliendelea kwa siri hadi mwezi Desemba 2025 ambapo mama yake mzazi aligundua kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi mitano.

Alipoulizwa kuhusu ujauzito huo, mhanga ndipo alimtambua mtuhumiwa Said Hemed Matuli kuwa ndiye aliyehusika. Ripoti ya uchunguzi wa DNA iliyoandaliwa baadaye ilithibitisha uhusiano huo