Haya Ndio Mashitaka 5 Yanayomkabili Aliyekuwa Mkurugenzi Wa Tbc Tido Mhando

Mkurugenzi wa Azam
Media, Tido Mhando amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo mashtaka manne ya Matumizi mabaya
ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya sh milioni 887.
Mhando
alifikishwa mahakamani hapo nyakati za asubuhi na ilipofika saa 5:22 asubuhi
aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kusomewa kesi yake hiyo.
Ilipofika
saa 11:44 asubuhi Hakimu Mkazi Mwandamizi,Victoria Nongwa aliingia mahakamani
hapo na Tido alipanda kizimbani.
Baada
ya Tido kupanda kizimbani, Mwendesha Mashtaka Wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akishirikiana na Aneth Mavika na Dismas
Mganyizi.
Akisoma
shtaka la kwanza Swai alidai kuwa Tido Juni 16,2008 katika maeneo ya Dubai,United
Arab Emirates(UAE) akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu kwa makusudi
alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya
utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 group
Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume na sheria ya manunuzi
kifungu namba31 na kuisabishia BVl kupata manufaa.
Katika
shtaka la pili Tido anadaiwa kuwa Juni 20,2008 katika utekelezaji wa kazi
yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano ya utangazaji wa digital
duniani kati ya TBC na BVl.
Katika
shtaka la tatu, Agosti 11,2008 na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Tido
anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano
wa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazi na mnara wa utangazaji kati
ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.
Shtaka
la nne, Tido anadaiwa kuwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai ,United Arab Emirates
alitumia vibaya madaraka yake kwa Kusini mkataba wa makubaliano(kuongea wakuu
wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji ( DTT broadcast
infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.
Katika
shtaka la tano Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,2008 katika
maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887,
122,219.19.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo,Tido ambaye anatetewa na wakili Ramadhani Maleta
alikana mashtaka yote.
Swai
alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hakimu
Nongwa alimtaka mshtakiwa hiyo kutoka fedha taslimu mahakamani hapo Sh 444
milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Mbali
na sharti hilo, pia awe na wadhamini wawili ambapo watasaini hati ya dhamana ya
maneno yenye thamani ya Sh 500 milioni na asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na
kibali cha mahakama.
Mshtakiwa
alikamilisha masharti hayo kwa kuwasilisha hati za mali na wadhamini wawili
nyakati za saa sita mchana na kuondoka.
Kesi
imeahirishwa hadi Februari 23,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).



