Tetesi Za Soka Barani Ulaya Leo Ijumaa

Na mashirika ya kimataifa
MSHAMBULIAJI wa Paris St-Germain na Brazil Neymar
ataruhusiwa kujiunga na Real Madrid, lakini kwa makubaliano ya iwapo ataisaidia
timu hiyo ya Ufaransa kubeba kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na rais wa
timu hiyo Nasser Al-Khelaifi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ana ndoto ya
kuichezea timu hiyo. (Goal)
Mazungumzo
yamegonga mwamba kati ya Arsenal na Borussia Dortmund kuhusu makubaliano ya
mshambuliaji wa klabu hiyo na Garbon Pierre -Emrick Aubameyang kwenda Arsenal.
Dortmund
pia inatarajiwa kusitisha majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal
Olivier Giroud .Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 anadaiwa
kutaka kushirikishwa katika kila mechi. (Mail)
Chelsea
inataka kumsajili Giroud , ikiwa na matumani ya kutaka kumshawishi kuhamia
magharibi mwa mji huo. (Mirror)
Manchester
City inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte
wikendi hii. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amebadilisha nia yake baada
ya kukataa uhamisho wa kueleka City miezi 18 iliopita.{Mirror}
Wakati
huohuo mmiliki wa Chelsea Abrahamovic amekasirishwa na mkufunzi Conte baada ya
kocha huyo kujitenga na usajili wa mchezaji mpya msimu huu. (Star)
Winga
wa PSG Brazil Lucas Moura, 25, alikutana na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy
mjini London siku ya Alhamisi kuzungumzia uhamisho wa kuelekea Spurs. (RMC - in
French)
Diafra
Sakho ameiambia West Ham anataka kuondoka na klabu ya Ufaransa ya Rennes ndio
anakoelekea . Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Senegal
hajashirikishwa katika mechi nyingi za West Ham msimu huu (Sun)
West
Ham inalenga usajili wa nahodha wa Fulham Tom Cairney na wako tayari kutoa dau
la £15m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Uskochi. (Sky
Sports)
West
Ham imewasilisha ombi la £12m kumsajili kiungo wa kati wa Norwich na Uingereza
James Maddison, 21. (Guardian)
Ombi la
pili la Crystal Palace kutaka kumsajili beki wa Lille Ibrahim Amadou
limekataliwa. Palace ilikuwa imehusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo wa
Cameroon mwenye umri wa miaka 24 mapema mwaka huu. (Sky Sports)
Mshambuliaji
wa zamani wa Fulham, Reading na Urusi Pavel Pogrebnyak, 34, alichiliwa na
Dynamo Moscow kwa sababu ya kuhudhuria mechi ya Juventus nchini Itali , licha
kuambia klabu hiyo kwamba alikuwa mgonjwa sana kuichezea (Sport Express - in
Russian)
Mshambuliaji
wa Leicester na Uingereza Jamie Vardy anatarajiwa kukabiliana na ,mwanafunzi
aliyehitimu kutoka chuo chake cha soka cha V9 Academy, Alex Penny, wakati
Leicester itakapocheza dhidi ya Peterborough katika kombe la FA raundi ya nne
siku ya Jumamosi. (Sky Sports)
Mkufunzi
wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa angependelea kufanyakazi katika
shamba badala ya kuifunza Arsenal au Barcelona , lakini raia huyo wa Argentina
ambaye ana umri wa miaka 45 hajapinga kuelekea Real Madrid.(Express)
Arsenal
wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Corinthians na mchezaji wa timu ya
Brazil isiozidi umri wa miaka 20 Maycon, 20. (Sun)
Mkufunzi
wa Leicester Claude Puel anasema kuwa winga Riyad Mahrez hatahamia klabu
nyengine yoyote wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 26 kutoka Algeria alipigwa picha akiwa katika uwanja wa
Emirates akitazama mechi ya kombe la Carabao kati ya Arsenal na Chelsea siku ya
Jumatano, lakini Puel amesisitiza kuwa anawatafutia wachezaji Leicester.
(Mirror)
Sandro
Ramirez ameambia Everton anataka kuondoka katika klabu hiyo. Mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 22 kutoka Uhispania yuko tayari kurudi nyumbani huku klabu
ya La Liga ya Sevilla ikimnyatia. (Mail)
Kiungo
wa kati wa West Brom na Ireland Kaskazini Chris Brunt, 33, anakaribia kusaini
kandarasi mpya katika klabu hiyo.(Birmingham Mail)



