KAULI YA POLEPOLE BAADA YA ASKOFU KAKOBE KUITWA NA IDARA YA UHAMIAJI

Baada ya watu mbalimbali kutoa maoni
yao juu ya kuitwa kwa Askofu Kakobe na idara ya Uhamiaji kuhojiwa Uraia wake,
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole ameandika yafuatayo kwenye
ukurasa wake wa Twitter; “Mbona kuhojiwa jambo la kawaida? baadhi ya watu
wanajenga tabia ya hovyo sana”
“Watu “wakubwa” wakiitwa kuhojiwa
inaonekana kitu cha ajabu. Mbona huku mtaani kuhojiwa Polisi ni kitu cha
kawaida tu, tuanze kuzoea na hasa ktk awamu ya 5 kwamba, na tunasisitiza
binadamu wote ni sawa” .




