Breaking News

MSUYA APINGA UTEUZI WA STEVE NYERERE KUWA MSEMAJI WA WASANII

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii na Waimbaji Nyimbo za Gospel nchini, Bw. David Msuya Ameelezea kutokuunga mkono hatua ya chama cha wasanii wa mziki kumchagua Steve Nyerere kuwa msemaji wa chama hicho.

Akizungumza jijijini dar es salaam alisema kimsingi hatua chama kumchangua steve kuwa msemaji wake sio kuwa tu aina ya tija kwa wasanii na wanachama bali pia ni moja ya kuonyesha jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wa chama hicho kukosa umakini.

"Binafsi siungi mkono hatua ya chama kumchagua Steve kuwa msemaji na niseme kwa hili viongozi wanatakiwa kujitathimini wenyewe juu ya utendaji wao kutokana na kushindwa hata kufanya utafiti Kuweza kupata msemaji"

Alisema nafasi hiyo inataka mtu mwenye kuwa na uelewa wa anacho kizungumzia pamoja na kuwa kama daraja la kutoa na kusemea mambo yanayoigusa tansia ya mziki nchini hivyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo ingekuwa vizuri kufanya utafiti wa kina hili kuweza kupata mtu ambae ataweza kufikia malengo ya wasanii.

"Binafsi na shauri ufanyike utafiti wa kina kwa kushirikisha na wasanii hususani wa mda mrefu na wenye weredi kuona namna ambavyo wanaweza kupata ushauri mzuri wa namna ya kufanya ili kupata kiongozi ambae ataweza kuwa kuwaunganisha wasanii na kusemea maslahi yao"