TAMASHA LA UTULIVU EXPERIENCE FESTIVAL KUENZI AMANI NA UTULIVU KUFANYIKA APRIL 20 JIJINI DAR
Taasisi ya Utulivu Space inatarajia kufanya uzinduzi wa Tamasha linalijulikana kama Utulivu Experience lenye lengo la kuwaletea pamoja watanzania kwa ajili ya kufurahia Utulivu na amani ambayo ni tunu ya Taifa tangu Tanzania ipate Uhuru.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Leo Jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, bwana Ibrahim Rwegerera amesema Tamasha hilo litakalofanyika April 20 katika ukumbi wa Super Dome Masaki limelemga kuwaleta pamoja watanzania kufurahia tuzo ya amani na utulivu tulionayo nchini
Alisema Tamasha hilo litawaleta pamoja na kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali ikiwemo watu maarufu, viongozi wa serikali, viongozi wa dini pamoja na watu wenye matokeo chanya Ndani ya Jamii.
"Wageni waalikwa katika tamasha hilo watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu na viongozi mbalimbali ikiwemo wastaafu na wale waliosaidia katika kudumisha amani na mshikamano wa Taifa" Alisema Bw.
Rwegerera.
Amesema kupitia Tamasha hilo washiriki watasherehekea faida za amani na Utulivu ambayo Moja ya alama inayolitambulisha taifa la Tanzania Duniani kote.
Bwana Rwegerera aliongeza kuwa kupitia jukwaa Utulivu Experience washiriki pia watapata wasaa kufurahia Neema za Mungu kama amani na Utulivu tulionao toka enzi za Wazee wetu ambao pia watapata wasaa wa kutoa uzoefu wao juu ya njia walizotumia kudumisha amani ambayo mpaka leo tunayo.
Alizungumzia viingilio siku ya Tamasha hilo alisema vitakuwa katika makundi matatu ambayo ni sehemu ya watu wa kawaida ni shilingi 270,000, VIP 1,350,000 na VVIP 2, 270,000.
Mapema akielezea maandalizi ya tamasha hilo bwana Antony Luvanda ambaye ni Mshauri wa Tamasha hilo amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake napemda kutoa wito kwa watanzania na raia wa nchi jirani kujumuika pamoja kuendelea kudumisha amani na Utulivu.
"Napenda kutoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wiki siku ya tarehe 20 April kuja kujionea wenyewe namna ambavyo tamasha hilo lilivyo bora ikiwa ni pamoja kuweza kujifunza mambo mengi kuhusu amani, umeoja na mshikamano wetu kama watanzania" Alisema Bw. Luvanda





