Breaking News

BALOZI NCHIMBI ABORESHA TAARIFA ZAKE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

.Dodoma, 20 Mei 2025 – Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo amejiandikisha kwa ajili ya kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. Zoezi hilo limefanyika katika kituo cha uandikishaji kilichopo Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kilimani, Mtaa wa Kilimani, jijini Dodoma.

Dkt. Nchimbi alifika kituoni hapo mapema leo asubuhi, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi ujao. Katika hotuba yake fupi kwa waandishi wa habari, alisisitiza umuhimu wa kila raia mwenye sifa kuhakikisha anaboresha au kuandikisha taarifa zake ili kutumia haki yake ya kidemokrasia kuchagua viongozi.

Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).