Breaking News

BASHUNGWA ATOA SIFA NA ZAWADI KWA ASKARI NA WATUMISHI, ASISITIZA UWAJIBIKAJI NA KUJITUMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amesema Serikali inatambua na kuthamini utendaji kazi wa Wakuu wa Vyombo vya Usalama, maafisa, askari na watumishi raia kwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na uwajibikaji wa hali ya juu katika kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na utulivu, amani na usalama.

Bashungwa ameeleza hayo katika hafla ya kutoa sifa na zawadi kwa askari, wanamichezo na wafanyakazi bora wa vyombo vya usalama na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2025, iliyofanyika tarehe 27 Mei 2025, jijini Dodoma.
"Nitumie fursa hii kuwapongeza askari na watumishi raia kwa kazi nzuri mnayoifanya. Mafanikio ya utulivu, amani na usalama tuliyonayo ndani ya taifa letu yanatokana na juhudi za kila mmoja wenu," amesema Bashungwa.

Bashungwa amewataka viongozi wa wizara, wakuu wa vitengo, wakuu wa vyombo, pamoja na wakuu wa mashirika na taasisi zilizo chini ya wizara kuendelea na utaratibu wa kuthamini na kutambua mchango wa watumishi sehemu za kazi.