Breaking News

WAZIRI SILAA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI KUTOKA DUBAI

Dodoma – Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.), amefanya mazungumzo na wawekezaji wa masuala ya mawasiliano kutoka kampuni ya United Advocates yenye makao yake makuu Dubai. Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dodoma.

Lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili fursa za ushirikiano katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari nchini Tanzania, hususan katika kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na kuongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali kwa wananchi.
Mhe. Silaa amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wawekezaji binafsi kutoka nje ya nchi katika kuhakikisha maendeleo ya haraka ya sekta ya mawasiliano, ambayo ni kiini muhimu cha uchumi wa kidijitali.

Wawekezaji kutoka United Advocates wameonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya kimkakati, ikiwemo ile ya kuongeza upatikanaji wa huduma za intaneti na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma kwa umma.