MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI NA VYA KATI 2025
Wanafunzi 149,818, sawa na asilimia 69.96%, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2025, huku wengine 64,323 wakipangiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu.
Takwimu hizo zimetolewa leo, Juni 6, 2025, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa. Amesema jumla ya wanafunzi 214,141 walikuwa na sifa za kuchaguliwa kuendelea na elimu ya juu ya sekondari na mafunzo ya ufundi, ambapo kati yao wasichana ni 97,517 na wavulana 116,624. Aidha, wanafunzi 1,028 kati yao ni wenye mahitaji maalumu.
Waziri Mchengerwa amesema zoezi hilo limezingatia vigezo vya ufaulu, nafasi zilizopo na usawa wa kijinsia, huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanajiunga na masomo au mafunzo kwa wakati.
bofya hapa kupata Majina www.tamisemi.go.tz au www.nactvet.go.tz




